Hospitali ya rufaa Alkafeel inagawa viti-mwendo awamu ya pili kwa wanajeshi waliojeruhiwa

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel imegawa viti-mwendo vilivyo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa wizara ya mambo ya ndani ili wapewe wanajeshi waliojeruhiwa.

Mkuu wa hospitali ya Alkafeel Dokta Jasim Ibrahimi amesema: “Tumegawa viti-mwendo awamu ya pili kwa wanajeshi majeruhi kutoka mkoa wa Diyala, Swalahu-Dini, Bagdad na Karbala”.

Akaongeza kuwa: “Zowezi hili linatokana na maelekezo ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi, ambae anahimiza kusaidia familia za mashahidi na majeruhi kwa kuwapa huduma za afya na zinginezo kuwa miongoni mwa vipaombele”.

Akabainisha kuwa: “Kujitolea walikofanya wanajeshi hakuwezi kulipwa kwa thamani yeyote, tunachotoa leo ni kidogo sana ukilinganisha na kazi kubwa waliyofanya ya kupambana na magaidi”, akasema: “Jamii ya raia wa Iraq ilipitia wakati mgumu sana hasa wale waliokua mstari wa mbele vitani”.

Majeruhi wameshukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na hospitali ya Alkafeel, wakasisitiza kuwa wamepewa huduma nzuri sana katika hospitali hiyo na imekua msaada mkubwa kwa jamii bila ubaguzi wowote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: