Usomaji wa Qur’ani tukufu ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mwezi mtukufu, mwezi wa Mwenyezi Mungu ambao waumini wameitwa katika ugeni wake, watu wanahudhuria kwa wingi katika vikao vya usomaji wa Qur’ani ndani ya ukumbi wa haram tukufu ambapo husomwa juzuu moja kila siku.
Kwa kuwa Qur’ani ni tulizo la nyoyo, na msimu wake ni mwezi wa Ramadhani, kutokana na kauli ya Mtume (s.a.w.w) isemayo: (Atakaesoma ndani ya mwezi wa Ramadhani aya moja ya Qur’ani ataandikiwa thawabu za kusoma Qur’ani yote katika miezi ngingine), utaona waumini wanahudhuria kwa wingi kwenye vikao vya usomaji wa Qur’ani ndani ya mwezi huu mtukufu.
Ushiriki wao kwenye vikao hivi vya usoamaji wa Qur’ani, unawawezesha kujifunza usomaji sahihi kwa kuzingatia hukumu za usomaji.