Maneno ya kuaga mwezi wa Ramadhani yamesikika kwenye minara ya malalo mbili takatifu kama ishara ya kukaribia kuisha kwa mwezi

Maoni katika picha
Wasomaji wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, wameimba kaswida za kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhani na sauti zao kusikika katika minara ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), karibu na wakati wa adhana ya Magharibaini, kama ishara ya kukaribia kuisha kwa mwezi huo mtukufu, mwezi wa ibada, mapenzi na rehema.

Kaswida za kuaga mwezi mtukufu huanza kuimbwa siku tatu kabla ya kuisha kwa mwezi, huo ni utamaduni uliozoweleka katika Ataba mbili tukufu, husomwa kaswida kwa sauti nyororo yenye hisia nzuri kwa msikilizaji na yenye huzuni kwa kuuaga mwezi bora mbele ya Mwenyezi Mungu.

Miongoni mwa maneno yaliyo sikika katika minara ya malalo mbili takatifu ni:

Kwa heri kwa heri.. ewe mwezi wa Ramadhani.

Kwa heri kwa heri.. ewe mwezi wa kisimamo.

Kwa heri kwa heri.. ewe mwezi wa twaa na msamaha.

Kwa heri kwa heri.. ewe mwezi wa wema na ihsani.

Huku ulimi wa mazingira ukisema: Tunatarajia Mwenyezi Mungu aurejeshe mwezi huu mwakani waumini wote wakiwa salama, hakika mwezi wa Ramadhani umeisha na unakaribia kutoweka, siku zake na saa zake zinamalizika, tunauaga na yawezekana tusikutane nao tena, na huenda tukakutana nao mwakani mwenyezi Mungu akitupa uhai, hakika alikua ni mgeni asiyekaa sana, amekaa siku za kuhesabika, hatukuhisi uwepo wake ispokua baada ya muda kuisha.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: