Sajili jina lako kwa ajili ya kufanyiwa ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku wa Iddi na mchana wake

Maoni katika picha
Idara ya program za msimu wa rehema inatoa wito kwa watu woto wa ndani na nje ya Iraq, wanaotaka kufanyiwa ziara ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku na mchana wa sikukuu ya Iddil-Fitri, ndani ya haram mbili takatifu wajisajili kupitia link ifuatayo: http://alkafeel.net/zyara.

Watakao fanya ziara ni wajukuu wa Zaharaa (a.s) wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu, nayo ni miongoni mwa program za mwisho katika mwezi wa Ramadhani zilizo anza tangu siku ya kwanza ya mwezi huu mtukufu.

Kumbuka kuwa ratiba hii ni miongoni mwa ratiba kubwa ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, nayo ni kufanya ziara kwa niaba ya kila atakaejisajili kwenye mtandao wa kimataifa Alkafeel kwa lugha yeyote miongoni mwa lugha zilizopo kwenye mtandao huo ambazo ni (Kiarabu, Kiengereza, Kifarsi, Kituruki, Kiurdu, Kifaransa, Kiswahili, Kijerumani), inahusisha ibada nyingi za mwezi wa Ramadhani, ikiwa ni pamoja na kutembelea malalo takatifu za Karbala na Najafu sambamba na usomaji wa Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: