Imeswaliwa asubuhi ya leo siku ya Jumatatu mwezi mosi Shawwal swala ya Iddil-Fitri, mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Imeswaliwa katika mazingira tulivu yaliyojaa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake pamoja na Ahlulbait (a.s), huku waumini wakiwa wamejaa haram mbili tukufu na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili.
Jamaa kubwa ya swala ilikua katika uwanja wa katikati ya haram mbili iliyo ongozwa na Mheshimiwa Sayyid Murtadha Qazwini.
Imeswaliwa pia ndani ya haram mbili tukufu zaidi ya mara moja, kutokana na wingi wa watu wanaokuja kuswali swala hiyo.
Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya kila iwezalo katika kulinda amani na kutoa huduma kwa mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), waliofika mapema kwa ajili ya kufanya ziara maalum ya Iddil-Fitri.