Chuo kikuu cha Al-Ameed kinahitimisha harakati zake za mwezi wa Ramadhani kwa kufuturisha mayatima

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kimehitimisha shughuli zake za mwezi wa Ramadhani kwa kufuturisha mayatima waliopo Karbala pamoja na walezi wao.

Rais wa kitengo cha maelekezo ya kinafsi na kimalezi Dokta Hassanaini Adnani Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Program zilizofanywa kwa usimamizi wa chuo ni moja ya harakati nyingi zilizofanywa na chuo kikuu hiki, ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, harakati hizo zinatokana na kuhisi kuwajibika katika jamii, na kujenga mapenzi na umoja kwa wanajamii, program hii imekua na athari kubwa kwa mayatima”.

Akaongeza kuwa: “Swala hili linatokana na kuwajali mayatima na kufanya shuguli za kuwakusanya kwa lengo la kujenga mapenzi baina yao na moyo wa kusaidiana”.

Mayatima na familia zao wameshukuru sana na wamepongeza program nzuri zinazofanywa na chuo kikuu cha Al-Ameed katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, wamemuamba Mwenyezi Mungu awape nguvu ya kuendelea kufanya program hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: