Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amemtembelea kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Husseiniyya Mheshimiwa Shekhe Abdulmahadi Karbalai katika mnasaba wa sikukuu ya Iddil-Fitri tukufu.
Sayyid Swafi amefuatana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ya uongozi, aidha alikuwepo pia katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya tukufu Sayyid Hassan Rashidi Al-Abaaiji.
Kikao chao kimekua na maneno mazuri ya kupongezana kutokana na kuingia kwa sikukuu ya Iddil-Fitri tukufu, na wakaangalia namna ya kuendelea kushirikiana baina ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, na njia za kuboresha kila kinacho husiana na kutoa huduma kwa mazuwaru watukufu.