Kamati ya maandalizi ya awamu ya pili ya shindano la maarifa ya turathi kwa vikundi katika mwezi wa Ramadhani, imepiga kura kwa ajili ya kuwapata washindi washindano hilo watakaopewa zawadi.
Kura imepigiwa katika ukimbi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kulikua na zaidi ya majibu (1000) yaliyo chujwa na kupata majibu sahihi yaliyopigiwa kura kwa ajili ya kupata washindi watatu.
Washindi watatu waliopatikana baada ya kura ni:
Mshindi wa kwanza: Mahmudu Kaadhim Jullah Khalf kutoka mkoa wa Bagdad, zawadi yake ni kwenda Umra.
Mshindi wa pili: Limyaa Jasim Kaadhim kutoka mkoa wa Bagdad, zawadi yake ni kutembelea malalo ya Imamu Ridhwa (a.s).
Mshindi wa tatu: Asawiru Azhar Hamudah kutoka mkoa wa Basra, zawadi yake ni kutembelea malalo ya bibi Zainabu (a.s).
Tambua kuwa gharama zote za ziara hizo zitatolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu.
Shindano liliandaliwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, vimeshiriki jumla ya vyuo vikuu kumi na mbili vya Iraq, kamati iliandaa maswali maalum ya shindano hilo.
Kumbuka kuwa kamati iliandaa zawadi za fedha kwa washindi watatu wa mwanzo, milioni tano dinari za Iraq kwa mshindi wa kwanza, milioni tatu dinari za Iraq kwa mshindi wa pili na milioni moja dinari za Iraq kwa msindi wa tatu.