Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kunyoosha mfupa wa paja wa mgonjwa mwenye umri wa miaka sabini baada ya kupungua (sm7).
Daktari bingwa wa mifupa katika hospitali hiyo Dokta Muhammad Saadi Haasir amesema: “Jopo la madaktari wetu limefanikiwa kunyoosha mfupa wa paja la mgonjwa mwenye umri wa miaka (70)”, akasema kuwa: “Kazi ya kuunyoosha imefanywa kwa kutumia teknolojia ya Ilizarov apparatus”.
Akafafanua kuwa: “Mgonjwa alikua na tatizo la upungufu wa mfupa wa paja kwa kiasi cha (sm7) kutokana na athari ya upasuaji aliowahi kufanyiwa zamani” akasisitiza kuwa: “Afya ya mgonjwa imeimarika baada ya kufanyiwa upasuaji huu katika hospitali ya rufaa Alkafeel”.
Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafaal inatoa huduba bora za matibabu kwa kutumia vifaa-tiba vya kisasa na madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi jambo ambalo limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa katika hospitali za kimataifa.
Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magonjwa tofauti, sambamba na kupokea wagonjwa wa aina mbalimbali walio katika hali tofauti za maradhi yao.