Kufanikiwa kwa ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi wa Ramadhani na Iddil-Fitri

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya umesema kuwa, ratiba zake za ulinzi, utumishi, afya na uratibu katika mwezi wa Ramadhani na siku za Iddil-Fitri zimepata mafanikio makubwa.

Ratiba zilizotekelezwa na vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi wa Ramadhani uliokuwa na idadi kubwa ya mazuwaru, hususan baada ya kutokua na wageni wengi kwa miaka miwili mfululizo kutokana na kuwepo kwa janga la virusi vya Korona.

Ratiba ilianza kutekelezwa toka siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani hadi siku ya Iddil-Fitri, zimepata mafanikio makubwa yaliyo tokana na juhudi na mshikamano wa watumishi wa Ataba tukufu na wahudumu wa kujitolea waliokuja kusaidia kazi, hakika kulikua na mpangilio mzuri wa utekelezaji wa majukumu na utoaji wa huduma kwa wageni wa malalo takatifu, hakukutokea tatizo lolote.

Hakika miongoni mwa sekta zilizopata mafanikio makubwa ni (Dini – Tablighi – Qur’ani – Utamaduni – Habari), na zinginezo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: