Kwa ushiriki wa wanafunzi 1000: Atabatu Abbasiyya inafanya hafla ya kuhitimu wanachuo wa kike hapa Iraq

Maoni katika picha
Idara ya shule za Alkafeel za wasichana katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya hafla ya kuhitimu kwa wanafunzi wa kike wa kiiraq kundi la (mabinti wa Alkafeel awamu ya nne), chini ya kauli mbiu isemayo: (Tunaangaza dunia kutokana na nuru ya Fatuma -a.s-)..

Hafla hiyo imehudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadha Dhiyaau-Dini, na kundi la wajumbe wa idara ya uongozi na marais wa vitengo, imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu iliyosomwa na Sayyid Hassanaini Halo, kisha ikasomwa surat Fat-ha na wimbo wa taifa sanjari na wimbo wa Ataba tukufu, halafu ukasomwa ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, amewapongeza wanafunzi kwa kufaulu katika masomo yao, pia amepongeza wazazi kwa malezi bora, kisha ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Ataba, ulio wasilishwa na mjumbe wa kamati kuu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi.

Tambua kuwa kazi kubwa imefanywa na vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, ya kufanikisha tukio hili kwa ufanisi mkubwa kama inavyo onekana.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: