Wanafunzi 1000 wa vyuo vikuu wanafanya hafla ya kuhitimu mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Wanafunzi 1000 kutoka vyuo vikuu tofauti vya Iraq wanafanya hafla ya kuhitimu masomo yao mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), asubuhi ya siku ya Jumamosi chini ya ratiba iliyopangwa na idara ya shule za Alkafeel za Dini tawi la wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu, hafla hiyo imefanywa chini ya kauli mbiu isemayo: (Tunaangaza dunia kutokana na nuru ya Fatuma -a.s-), kundi la nne la wasichana wa Alkafeel mwaka 2022 lahitimu masomo.

Hafla imefanyiwa kwenye uwanja wa mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), imehudhuriwa na kundi kubwa la viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na maraisi wa vitengo vyake, ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu, halafu ikasomwa surat Faatihah kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq.

Kikafuata kiapo cha kuhitimu mbele ya kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) kilicho ongozwa na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya Dokta Ahmadi Kaabi, kilikua kinasema: Naapa mbele ya Mwenyezi Mungu mkuu, nitatekeleza amana ya elimu kwa kutumikia taifa langu na kuheshimu mipaka ya Dini yangu kwa siri na hadharani..

Baada ya hapo ikasomwa ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa pamoja, iliyo ongozwa na mmoja wa masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya, halafu wanafunzi wakaenda kuzuru kaburi lake na kaburi la ndugu yake Imamu Hussein (a.s).

Wanafunzi wamefurahi sana kwa ratiba hii, wakasema kuwa kufanya hafla ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kusoma kwao kiapo ni msingi wa mabadiliko katika Maisha yao, wakaahidi kufanya kazi kwa uwezo wao wote katika kutumikia taifa hili, wameishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu na idara ya shule za Alkafeel kwa kuandaa ratiba hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: