Kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya warsha yenye anuani isemayo: (Mpangilio wa masomo) kwa watumishi wa kitengo hicho.
Ustadhi Haitham Imaad Twaiy amesema: “Warsha imeangazia ujazaji wa fom ya maelezo kwa kukamilisha masomo, na namna ya kupata matokea, sambamba na mambo yanayotakiwa kwa mtumishi”.
Akaongeza kuwa: “Maelekezo hayo yanahusu watumishi wa Ataba tukufu, chini ya usimamizi wa Ataba unaoendana na maendeleo ya kila sekta”.
Akafafanua kuwa: “Warsha imefanywa kwa muda wa saa (3), kwa ushiriki wa watumishi (14) kutoka idara tofauti”.
Kumbuka kuwa kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, huendesha warsha na semina za kielimu zinazo lenga kukuza uwezo wa watumishi wa Ataba tukufu katika sekta tofauti.