Ugeni kutoka uongozi wa mazaru ya bibi Sharifah mtoto wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) ukiongozwa na katibu mkuu wao Mhandisi Manadhil Ali Hassan umetembelea Atabatu Abbasiyya tukufu.
Baada ya kumaliza ibada ya ziara na dua mbele ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wamepokelewa na makamo rais wa kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya Sayyid Muhammad Jaluhani, amewakaribisha na kuwaeleza miradi inayofanywa na Ataba ya kuhudumia mazuwaru, pamoja na maeneo ya ushirikiano.
Naye Mhandisi Manadhil Ali Hassan na wageni aliokuja nao, wamepongeza kazi nzuri inayo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na watumishi wote, mwisho wa ziara wageni wameshukuru na kupongeza mapokezi mazuri waliyopewa na ukarimu waliofanyiwa.