Kukumbuka jinai ya uvunjwaji wa makaburi ya Baqii katika haram ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeadhimisha kumbukumbu ya uvunjwaji wa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s), ambako kunasadifu tarehe kama ya kesho Jumanne mwezi nane Shawwal (1443h), wamefanya majlisi ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na itaendelea kwa muda wa siku tatu.

Majlisi inaratibiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu kila mwaka, chini ya mradi wa Ummul-Banina (a.s), kupitia kitengo maalum cha kukumbuka na kuadhimisha matukio ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), likiwepo tukio hili ambalo lilitokea siku kama hizi la uvunjwaji wa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s).

Ratiba ya majlisi inahusisha utoaji wa mihadhara miwili, mhadhara wa asubuhi unatolewa na Shekhe Muhyi-Dini Al-Asadiy, alianza toka siku ya Jumapili mwezi sita Shawwal, mhadhara wa pili hutolewa jioni, unaratibiwa kwa ushirikiano na taasisiya (Al Baqee Organization), hutolewa baada ya swala ya Isha na Shekhe Muhammad Ni’mah kutoka Lebanoni, halafu hufuatiwa na majlisi ya (maatam), ambayo husomwa na muimbaji wa Husseiniy Baasim Karbalai, ataendelea kwa muda wa siku mbili kuanzia jioni ya Jumatatu mwezi saba Shawwal.

Kumbuka kuwa mwezi nane Shawwal ni kumbukumbu ya kuvunjwa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s), ambao ni: Imamu Hassan Almujtaba mtoto wa kiongozi wa waumini, Imamu Ali Zainul-Aabidina mtoto wa Hussein (a.s) na Imamu Muhammad Albaaqir mtoto wa Imamu Zainul-Aabidina, Imamu Jafari Swadiq mtoto wa Imamu Albaaqir (a.s), pale maadui wa nyumba ya Mtume walipo amua kuvunja makaburi hayo matukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: