Maombolezo na huzuni za Baqii katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Maombolezo na huzuni za Baqii katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kuhuisha na kukumbuka jinai ambayo jeraha lake halijapona hadi leo, nayo ni uvunjwaji wa makaburi ya Maimamu (a.s) na kuvunja heshima yao katika eneo hilo takatifu.

Watumishi wa kitengo cha kusimamia haram tukufu kwa kushirikiana na watumishi wa kitengo cha zawadi na nadhiri idara ya ushonaji katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamekua wakiweka mapambo meusi katika haram kwa zaidi ya siku mbili kama ishara ya kuonyesha huzuni kwa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w) na wafuasi wao iliyotokea mwezi nane Shawwal.

Kuta za haram tukufu zimewekwa mabango yanayolaani tukio hilo na kuandikwa ujumbe unaoashiria huzuni kwa tukio hilo baya pamoja na kumpa pole Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s).

Kumbuka kuwa mwezi nane Shawwal ni siku yaliyovunjwa makaburi ya Maimamu wa Baqii, ambao ni: Imamu Hassan Almujtaba mtoto wa kiongozi wa waumini, Imamu Ali bun Hussein Zainul-Aabidina, Imamu Muhammad bun Ali Albaaqir, Imamu Jafari Swadiqu bun Imamu Albaaqir (a.s), tukio hili ni kuadhimisha miaka tisini na tisa tangu maadui wa Ahlulbait (a.s) walipovunja makaburi ya Baqii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: