Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ndani ya ukumbi wa utawala asubuhi ya Jumanne, iliyo hudhuriwa na watumishi wake pamoja na baadhi ya mazuwaru wa Abulfadhil Abbasi (a.s), wameongea kuhusu kumbukumbu ya jinai zilizofanywa na maadui wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) kwa kuvunja makaburi ya Baqii katika siku kama ya leo, mwezi nane Shawwal miaka tisini na tisa iliyopita.
Majlisi ni sehemu ya ratiba ya uombolezaji iliyoandaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ilifunguliwa kwa Qur’ani iliyofuatiwa na muhadhara kutoka kwa Shekhe Muhammad Kuraitwi wa kitengo cha Dini, ameongea mambo mengi kuhusu tukio hilo na matatizo waliyopata Maimamu wa Ahlulbait (a.s) katika uhai wao na baada ya kufa kwao, walidhulumiwa wakiwa hai na bado wanaendelea kudhulumiwa hadi leo, makaburi haya matakatifu ya Baqii ni kielelezo hai cha dhulma walizo fanyiwa, yamevunjwa zaidi ya mara moja.
Majlisi ikahitimishwa kwa kusoma tenzi za kuomboleza tukio hilo la kuhuzunisha.
Kumbuka kuwa mwezi nane Shawwal ni kumbukumbu ya kuvunjwa kwa makaburi ya Maimamu wa Baqii (a.s), nayo ni kumbukumbu ya mwaka wa tisini na tisa tangu maadui wa Ahlulbait (a.s) wavunje makaburi ya Maimamu watakatifu (a.s): Imamu Hassan Almujtaba mtoto wa kiongozi wa waumini, Imamu Ali bun Hussein Zainul-Aabidina, Imamu Muhammad bun Ali Albaaqir, Imamu Jafari Swadiq mtoto wa Imamu Baaqir (a.s), na wake wa Mtume (s.a.w.w) na maswahaba wake watukufu waliozikwa Baqii katika mji mtukufu wa Madina.