Kutoa mualiko kwa wizara ya elimu ya juu na malezi wa kushiriki kwenye kongamano la utengenezaji wa App

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umekabidhi mualiko kwa wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu na wizara ya malezi, wa kuhudhuria na kushiriki kwenye kongamano la kijana mzalendo wa Alkafeel linalo husu utendenezaji wa App na roboti, kongamano hilo litafunguliwa siku ya Jumatano (9 Shawwal 1443h) sawa na tarehe (11 May 2022m).

Ugeni umeongozwa na Dokta Mushtaqu Abbasi Muan rais wa kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kitengo cha mahusiamo.

Kituo cha kwanza kuwasilisha mualiko ilikua wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, ugeni ulipokewa na Dokta Ali Hamidi Shukuri na kituo cha pili ikawa ni wizara ya malezi ambapo wageni wamepokewa na mtendaji mkuu wa ofisi ya Waziri Ustadh Sa’adi Abdul-Khadiir.

Wakati ugeni unakabidhi mialiko umefafanua kuhusu malengo ya kongamano na ratiba yake, na muitikio mkubwa unao onyeshwa na vyuo vikuu na idara za malezi, kutokana na wingi wa washiriki wanaojitokeza kwenye kongamano hilo, jumla ya vyuo vikuu (42) na idara za malezi (12) zinashiriki kutoka mikoa tofauti, washiriki hao watapewa nafasi ya kutoa ujumbe kwenye hafla ya ufunguzi.

Kumbuka kuwa kongamano linalenga kuangalia matokeo ya ubunifu wa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi, na uibuaji wa vipaji vyao, kongamano litakua na sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni warsha ya kitaalam kuhusu utambuzi, na sehemu ya pili shindano la kielimu linalo husu utengenezaji wa roboti, kunazawadi nzuri zilizo andaliwa na kamati ya maandalizi kwa washindi wa shindano hilo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: