Warsha imeongozwa na Dokta Yusufu Khalfu mkuu wa miradi katika wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu, mada zifuatazo zimewasilishwa:
- - (Utengenezaji wa Roboti, maendeleo endelevu ya kitengo cha shule na vyuo), mada hiyo imetolewa na Dokta Muhandi Haidari mkufunzi wa chuo kikuu cha Karbala/ kitengo cha kompyuta.
- - (Matumizi ya App za kisasa), imetolewa na Mhandisi Ammaar Hanun anayeishi Marekani mwenye asili ya Iraq, mbobezi wa mambo ya kompyuta.
- - (Utambuzi wa kibinaadamu, ni maangamizi au jambo zuri), imetolewa na Dokta Mustwafa Khalidi kutoka chuo kikuu cha Bagdag na Ali Zubaidi rais wa shirika la (STEAMERS) la Iraq.
Warsha imeshuhudia michango ya kielimu kuhusu maendeleo ya kisasa yaliyofikiwa duniani katika sekta ya roboti na intanet.