Kuhitimisha kongamano la kitaifa kuhusu App za kisasa na utengenezaji wa roboti na wito wa kufanyia kazi maazimio

Maoni katika picha
Jioni ya siku ya leo Alkhamisi kongamano la Multaqal-Kafeel la kitaifa kuhusu utengenezaji wa roboti na App za kisasa, lililo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha mahusiano idara ya (mahusiano ya vyuo vikuu na shule), ndani ya ukumbi wa Imamu Almujtaba (a.s) katika chuo kikuu cha Al-Ameed.

Imefanywa hafla ya ufungaji wa kongamano hilo iliyohudhuriwa na kiongozi wa ofisi ya Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Afdhalu Shami, na baadhi ya viongozi pamoja na wawakilishi wa wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu na wizara ya malezi, bila kusahau ugeni ulio wakilisha baadhi ya vyuo vikuu tofauti vya Iraq, na washiriki wa mashindano.

Hafla ya kuhitimisha kongamano imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, ikafuatiwa na ujumbe wa rais wa kamati iliyosimamia kongamano na mkuu wa kitengo cha miradi ya kielimu kutoka wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu Dokta Yusufu Khalfu Yusufu, akasisitiza kuwa Atabatu Abbasiyya imekua ikiibua wabunifu daima kupitia miradi yake, kongamano hili ni dalili ya wazi ya mafanikio yake, ni kongamano la aina yake ambalo limefanywa kwa mara ya kwanza hapa Iraq, limekusanya wasomi kutoka wizara ya elimu ya juu na malezi, ambao wamejadili App za kisasa na utengenezaji wa roboti.

Halafu yakatangazwa majina ya watu walioshinda kwenye mashindano yaliyofanywa kama ifuatavyo:

Wanafunzi wa vyuo vikuu walioshinda:

Kwanza: kutengeneza roboti linalo endeshwa kwa hewa (bila waya), mwanafunzi Muhandi Shaakir Muhammad kutoka chuo kikuu cha Mustanswiriyya.

Pili: kutengeneza ndege isiyokua na rubani, mwanafunzi Ismaili Liith kutoka chuo kikuu cha Iraaqiyya.

Tatu: kutengeneza kofia ngumu (helment) tambuzi, mwanafunzi Hassan Haadi Khadhar kutoka chuo kikuu cha Kuut.

Walioshinda miongoni mwa wanafunzi kutoka wizara ya malezi:

Kwanza: kutengeneza mtambo wa (CNC) wa kuonyesha maeneo (ramani), mwanafunzi Leeth Muhammad Twaariq kutoka mji wa Karkhi tatu.

Pili: roboti linalotembea kwa kufuata mstari, mwanafunzi Zainabu Ali Shammaai kutoka mji wa Karkh tatu.

Tatu: barakoa tambuzi, mwanafunzi Ali Zainu-Dini Ahmadi kutoka idara ya malezi ya mkoa wa Nainawa.

Tatu aliyefungana: mradi wa usambazaji wa wanyama wafugwao, mwanafunzi Mustwafa Iswaam kutoka kituo cha malezi cha Raswafa.

Baada ya hapo watu wote walioshinda kwenye mashindano wakapewa zawadi sambamba na kuwapa zawadi kamati ya maandalizi na muwakilishi wa wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu na wawakilishi wa vyuo vikuu na wizara ya malezi na ofisi zilizo chini yake bila kusahau kamati iliyowezesha kufanikiwa kwa kongamano hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: