Matawi ya Ataba takatifu za Iraq yanamuonekano wa pekee katika maonyesho ya vitabu kimataifa jijini Teheran

Maoni katika picha
Matawi ya Ataba takatifu za Iraq Alawiyya, Husseiniyya na Abbasiyya zinazo shiriki kwenye maonyesho ya vitabu yanayoendelea hivi sasa jijini Teherani, zinamuonekano wa pekee katika upangiliaji na aina ya vitabu walivyo navyo.

Kiongozi wa tawi la Atabatu Alawiyya Ustadh Haidari Mussawi amesema: “Tumeshiriki tukiwa na zaidi ya aina mia mbili za vitabu pamoja na majarida ya najafu ya zamani kuanzia mwaka wa (1905m) hadi mwaka (1965m), machapisho (70) yanayo husu historia ya kiongozi wa waumini (a.s), machapisho (45) yameandikwa mambo mbalimbali ya kijamii katika lugha tofauti”, akaongeza kuwa “Lengo la kushiriki kwetu kwenye maonyesho haya ni kusambaza fikra na utamaduni wa Ahlulbait (a.s)”.

Naye rais wa kitengo cha habari katika Atabatu Husseiniyya tukufu Ustadh Ali Bashiri amesema: “Tumeshiriki maonyesho haya tukiwa na aina (600) za vitabu vya Fiqhi, Aqida, Tafsiri ya Qur’ani, vitavu vinavyo elezea maisha ya Imamu Hussein (a.s) na majarida mbalimbali”.

Akaongeza kuwa: “Tawi letu kwa kushirikiana na tawi la Atabatu Abbasiyya yanafanya mashindano ya kifikra kwa watu wanao tutembelea, pamoja na fikra za utii ziitwazo (Barua kwenda kwa kaburi la Imamu Hussein a.s)”.

Kuhusu matawi ya Ataba za Iraq, kiongozi wa tawi la Atabatu Abbasiyya Ustadh Haidari Twalibu Mamitha amesema: “Awamu hii matawi ya Ataba takatifu yamepangwa kwa utaratibu unaoendana na malalo tukufu, kutokana na kuwepo kwa muonekano wa picha za malalo, kunatia athari nzuri katika nafsi za watu wanaokuja kutembelea maonyesho, aidha unaonekana wazi umuhimu wa uwepo wetu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: