Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya program ya (kisimamo) kwa kushirikiana na idara ya askari wa usalama barabarani katika mkoa wa Karbala

Maoni katika picha
Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya program ya (kisimamo) kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na idara ya usalama na ukumishi katika mkoa wa Karbala, ili kuwatia moyo na kuongeza hamasa katika kutekeleza majukumu yao hasa askari wa usalama barabarani.

Kiongozi wa idara ya mahusiano na mawasiliano ya ndani Ustadh Rasuul Naaji ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu na uongozi wa kitengo husika, tumefanya program ya (kisimamo) kwa kushirikiana na idara ya usalama barabarani na utumishi katika mkoa wa Karbala, idara hiyo tumekua na ushirikiano toka zamani, lakini hii ni program maalum ambapo tutashirikiana nao wakati wote”.

Akaongeza kuwa: “Sehemu yetu ya kwanza katika program yetu tumekutana na mkuu wa askari wa usalama barabarani katika mkoa wa Karbala, kikosi chetu kimemtembelea mkuu wa kitengo cha usalama barabarani pamoja na askari waliokua zamu”.

Akabainisha kuwa: “Tumewasilisha salamu za kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (a.s), na kuwataka waendelee kuhudumia wananchi na mazuwaru, na kuhakikisha wanaonyesha picha nzuri kwa wageni kupitia huduma zao, jambo hilo limezoweleka kwao, aidha wamepewa zawadi za kutabaruku kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), zawadi hizo zimekua na athari kubwa kwao”.

Kwa upande wao askari wa usalama barabarani, wameshukuru Atabatu Abbasiyya na wahudumu wake kwa kuwatembelea na kuwapa zawadi, wakasema kuwa hili sio jambo geni kwao, hakika Ataba imekua mstari wa mbele kusaidia askari wa usalama barabarani na kuhimiza wananchi kutii sheria na kanuni, bila shaka ziara hii imeongeza hamasa kwa askari wa usalama barabarani ya kuendelea kutumikia wananchi na mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: