Shindano la kitamaduni ni jambo la pekee katika tawi la Atabatu Abbasiyya kwenye maonyesho ya vitabu kimataifa jijini Tehran

Maoni katika picha
Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na Atabatu Husseiniyya kwenye maonyesho ya vitabu jijini Tehran linaendesha shindano la kifikra kwa watu wanaotembelea maonyesho hayo.

Shindano linamaswali mengi ya kifikra na kihistoria, yameandikwa kwenye karatasi ambayo anapewa mtu anayependa kushiriki kwenye shindano hilo, na baada ya kuandika majibu karatasi hiyo inawekwa kwenye sanduku maalum.

Siku ya mwisho wa maonyesho zitapigwa kura kwa ajili ya kupata washindi sita watakao pewa zawadi ya kwenda kufanya ziara kwenye malalo mbili ya bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) huko Karbala.

Hili ni jambo la pekee linalofanywa na matawi ya Ataba mbili tukufu kwenye maonyesho haya, limepata muitikio mkubwa kutoka kwa wadau wa maonyesho.

Shindano hili ni sehemu ya malengo ya Ataba mbili takatifu katika kueneza fikra za Ahlulbait (a.s) na utamaduni wa kidini katika jamii ya kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: