Usanifu wa pekee na umakini wa utekelezaji.. kazi ya kutengeneza dirisha la bibi Zainabu (a.s) inaendelea

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo cha utengenezaji wa madirisha ya makaburi na milango mitukufu katika Atabatu Abbasiyya wanaendelea na kazi ya kutengeneza dirisha la bibi Zainabu (a.s) kama ilivyo pangwa, wanafanya kazi kwa umakini mkubwa na kuhakikisha wanafikia kilele cha uzuri.

Rais wa kitengo Sayyid Nadhim Ghurabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kazi inayo endelea kwa sasa ni kutengeneza sehemu za madini zilizobaki kwenye dirisha, ambazo ni sehemu muhimu kwenye dirisha hilo, linalotengenezwa kwa umakini na ustadi mkubwa, sambamba na kumalizia sehemu zingine na kuanza kudhihiri muonekano wake halisi siku baada ya siku”.

Akaongeza kuwa: “Dirisha hilo linasehemu tofauti za madini, kila sehemu ya madini inayokamilika unaunganishwa kwenye dirisha moja kwa moja, kazi hii itaendelea hivyo hadi itakapo kamilika yote kwa idhini ya Mwenyezi Mungu”.

Ghurabi akasisitiza kuwa: “Sehemu za madini zinazo tengenezwa asilimia kubwa ni sehemu za nakshi na mapambo ya kutengenezwa kwa mikono, kazi hiyo inahitaji umakini mkubwa sambamba na nakshi na mapambo yaliyopo sehemu zingine za dirisha, ifahamike kuwa nakshi na mapambo hayo yanafanana na yale yaliyopo kwenye dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akamaliza kwa kusema: “Vipande vya madini vinatengenezwa kwa madini ya dhahabu, fedha na shaba, ujazo wa madini hayo unatofautiana kutokana na kutofautiana kwa vipande husika”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: