Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki kwenye kungamano la mahusiano ya kimataifa

Maoni katika picha
Asubuhi ya Jumamosi ndani ya haram tukufu ya malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) limefanyika kongamano la kujadili mahusiano ya kimataifa, lililo hudhuriwa na wawakilishi wa Ataba na mazaru za ndani na nje ya Iraq lenye lengo la kuimarisha mawasiliano kati yao kwa ajili ya kuboresha huduma kwa mazuwaru watukufu.

Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye kongamano hilo imewakilishwa na makamo kiongozi mkuu wa mahusiano Sayyid Muhammad Jalukhani, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika kushiriki kwenye kongamano linalosimamiwa na Atabatu Alawiyya, kunaimarisha ushirikiano kati ya Ataba tukufu na mazaru, kwa lengo la kuboresha huduma kwa mazuwaru wa malalo takatifu na kujadili nyenzo zinazoweza kusaidia uboreshaji huo”.

Akaongeza kuwa: “Washiriki wamewasilisha maoni yao na mapendekezo, kisha yakajadiliwa na kuandaa maazimio”.

Tumeongea na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi katika Atabatu Alawiyya Dokta Salim Jaswani kuhusu umuhimu wa kongamano hili, amesema: “Kongamano la mahusiano ya kimataifa linasaidia kujenga mapenzi na ushirikiano katika kuwahudumia mazuwaru”.

Akaongeza kuwa: “Muwakilishi wa Ataba na mazaru ameshauri kupanua wigo wa kongangamano kwa kushirikisha nchi ambazo hazijashiriki kwenye kongamano hili, sambamba na kuboresha huduma, tunatarajia kufanya kongamano lingine siku zijazo pamoja na kusoma maazimio na kuandaa kamati”.

Wageni waliokuja kushiriki kwenye kongamano hili wamefanya ziara ndani ya ukumbi wa haram ya kiongozi wa waumini pamoja na watumishi wa malalo hiyo takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: