Maahadi ya wahadhiri wa Husseiniyya imeanza kupokea maombi mapya

Maoni katika picha
Maahadi ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya imeanza kupokea wanafunzi wapya wa mwaka wa masomo 2022 wanaopenda kujiunga na mimbari ya bwana wa mashahidi (a.s) chini ya utaratibu uliopangwa.

Mkuu wa Maahadi bibi Taghrida Tamimi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumefungua ukurasa wa kujisajili kwa njia ya mtandao kila msichana anaependa kusoma, baada ya kuisha muda wa kujisajili kutawasiliana na waliojisajili na kuwapokea katika ofisi za Maahadi zilizopo kwenye jingo la Swidiqah-Twahirah katika mkoa wa Karbala kwa ajili ya kukamilisha mchakato wa usajili”.

Akaongeza kuwa: “Wale walio jisajili kwa njia ya mtandao wanapokuja kwenye ofisi zetu hupewa fomu maalum za kukamilisha usajili wao kwa kuandika taarifa zao, kisha huingia ukumbini kwa ajili ya kupewa maelekezo, halafu hupewa mtihani wa jaribio, ili kubaini uwezo wao”.

Akabainisha kuwa: “Wanafunzi wanaofaulu jaribio hilo hupokelewa na kuanza kufundishwa masomo ya msingi, ambayo ni Aqida, Uhadhiri, Nahau, Ibadaat, Twahara, Tafsiri ya Qur’ani, Usomaji wa Qur’ani, Historia ya Mtume pamoja na kusikiliza mihadhara inayokidhi vigezo vya kielimu”.

Kumbuka kuwa muda wa masomo ni miaka mitatu, sambamba na kupewa nafasi ya kufanya Tablighi kila mwaka, kutokana na umuhimu wa swala hilo hususan wakati wa msimu wa maombolezo, na kuongea sehemu za watu wengi, kwa lengo la kufikisha ujumbe wa Husseiniyya wa milele kwa njia nzuri inayo eleweka kwa urahisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: