Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kuweka ukanda wa kijani katika mkoa wa Karbala wenye ukubwa wa mita 2,700,000.

Maoni katika picha
Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanao fanya kazi katika ukanda wa kijani kusini ya mkoa wa Karbala, wanafanya kazi kubwa ya kurudisha muonekano wa kijani, ukizingatia kuwa kufanya hivyo ni kuboresha mazingira ya mji, na kupunguza athari zinazo weza kutokea kutokana na uharibifu wa mazingira, kama vile kimbunga nk.

Mkuu wa mradi huo, Ustadh Nasoro Hussein Mut’ibu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika Atabatu Abbasiyya tukufu imeweka mkakati Madhubuti wa kurudisha muonekano wa kijani katika ukanda huu kutokana na umuhimu wake, tumemaliza hatua muhimu katika mradi huo, ambayo ni kukarabati pampu za kusukuma maji zipatazo (49), kila pambu inauwezo wa kumwagilia sehemu ya shamba na kuweka maji kwenye hodhi kwa ajili ya umwagiliaji, aidha tumetoa miti ya zamani na kupanda miti mipya inayo hitajika katika ukanda huu”.

Akaongeza kuwa: “Ukanda wa kijani katika upande wa kusimu unaurefu wa kilometa (27) na upana wa (mt 100), tunafanya kazi kwa hatua, tumemaliza hatua ya kwanza, tunaendelea kukamilisha hatua zilizo baki, hadi tufikie malengo yaliyo kusudiwa kiuchumi, kimazingira na kijamii, tambua kuwa mradi huu unasaidiwa moja kwa moja na Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akabainisha kuwa: “Ukanda huo umepandwa aina tofauti za miti kwa mistari, kwenye eneo lote lenye ukubwa wa mita (2,700,000), kuna miti ya mitende, mizabibu, misonobari na miti ya mauwa”.

Kumbuka kuwa mradi wa kutengeneza ukanda wa kijani unaofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ni sehemu ya mkakati wa kuweka mazingira mazuri katika mkoa wa Karbala, aidha ni miongoni mwa miradi ya kimkakati katika utunzaji wa mazingira sambamba na umuhimu wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: