Kituo cha turathi za Hilla kimeangazia tafiti za Shekhe Ibun Idrisa Alhilliy (q.s)

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa kitabu cha (Almabaahithu Rijaliyyah fii turathi Sheikhe Muhammad bun Idrisa Alhilliy) kilicho andikwa na Sayyid Haidari Watuut Alhusseiniy.

Mkuu wa kituo Shekhe Swadiq Khawilidi ameuambia mtandao wa Almafeel kuwa: “Shekhe Ibun Idrisa Alhilliy aliyefariki kwaka (598h), ni mwanachuoni mkubwa katika madhehebu ya Imamiyya, kutokana na mchango mkubwa wa kielimu aliotoa baada ya Shekhe Tusi aliyefariki mwaka (460h), shekhe ameandika kwenye nyanja nyingi ikiwemo Ilmu-Rijaali, japokua hakua na kitabu rasmi cha somo hilo”.

Akaongeza kuwa: “Hivyo muandishi wa kitabu hiki amejaribu kubainisha sekta hiyo kupitia nakala zilizo andikwa na Shekhe, kwenye kitabu chenye kurasa (272), mambo muhimu yaliyomo kwenye kitabu hicho ni: maelezo yake kwa kina katika mlango wa kwanza na kazi za kalamu yake, katika mlango wa pili ameandika (mabaani-rijaaliyya) kwa upande wake, matamshi ya riwaya, kauli zake kwa wapokezi, pamoja na kubainisha sehemu zinazo kubaliana na kutofautiana na mtazamo wa walio mtangulia miongoni mwa wanachuoni wa fani hiyo, sambamba na faharasi mbalimbali zinazoonyesha matni za masomo”.

Akafafanua kuwa: “Muandishi katika mpangilio wake kwenye turathi ya rijali ametegemea (Mausua ya Ibun Idrisa Alhiliy) kwa uhakiki wa Allamah Muhammad Mahdi Khurasani wa mwaka 2008m”.

Akasisitiza kuwa: “Kitabu hiki kinaelimu kubwa sambamba na mnyambuliko wa kielimu wenye mtazamo wa wanazuoni wa Hilla na mitazamo yao katika mambo mbalimbali”.

Anaetaka kuona kitabu hicho atembelee maonyesho ya vitabu ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: