Watu wanaendelea kutembelea tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye maonyesho ya vitabu kimataifa yanayoendelea jijini Tehran

Maoni katika picha
Watu wanaotembelea maonyesho ya vitabu kimataifa katika jiji la Tehran, awamu ya thelathini na tatu, wanaendelea kumiminika katika tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu kuangalia machapisho yake.

Tawi letu limepata muitikio mkubwa kutoka kwa wadau wa maonyesho kutokana na umuhimu wa vitabu tulivyo navyo, na kushiriki shindano la kitamaduni linalo endeshwa na tawi pamoja na kipengele cha kuandika barua kwa kaburi.

Tawi limeshuhudia ushiriki wa mamia ya mazuwaru kwenye shindano la kielimu, pamoja na mamia ya barua zinazotumwa kwa kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s).

Tambua kuwa maonyesho ya vitabu kimataifa jijini Tehran yanafanywa kwa mara ya thelathini na tatu, kwa muda wa siku kumi, kuanzia tarehe (11 – 21 Mei 2022m).

Kumbuka kuwa kushiriki kwenye maonyesho ya vitabu ya kimataifa ni miongoni mwa mambo muhimu yanayo isaidia Atabatu Abbasiyya tukufu kujiweka wazi katika ulimwengu wa kiislamu, na kutambulisha mafanikio yake kielimu na machapisho yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: