Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa mtazamo wake kuhusu muathiri na nafasi yake katika Maisha ya mwanaadam

Maoni katika picha
Kituo cha utafiti na mambo ya kielimu chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa mtazamo wake kuhusu muathiri na nafasi yake katika Maisha ya mwanaadamu na jamii.

Jambo hilo limefanywa kwenye nadwa ambayo mtoa mada alikua ni mkuu wa kituo hicho Ustadh Hassan Aljawaadi mbele ya vijana wa mtaa wa Twali’a katika mkoa wa Baabil, mada yake ilikua inasema: (Nafasi ya muathiri katika Maisha ya mwanaadamu na jamii tunayoishi).

Ameongea kuhusu umuhimu wa muathiri katika Maisha ya mwanaadamu na umuhimu wa mwanaadamu kupima viashiria vinavyo weza kumuathiri bila kujitambua au kuona ukubwa wa ubaya wake.

Akafafanua kuwa, mwanaadamu anatakiwa kufanya juhudi ya kukamilisha nafsi yake, kwa kuielekeza kwenye muongozo wa kisheria na hekima za kiakili, wala sio kuiingiza kwenye matamanio na mambo yasiyofaa.

Nadwa hiyo imefanywa kwa mara ya kwanza katika mtaa huo na imepata muitikio mkubwa, imepambwa na maswali pamoja na maoni mazuri kutoka kwa washiriki, wamepongeza kazi zinazofanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya kujenga uwelewa na fikra sahihi kwa vijana wenye umri tofauti.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: