Kuanza kwa ratiba ya hafla za Arshu-Tilaawah katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeanza kufanya hafla za Arshu-Tilaawah ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Wasomaji wa Ataba tukufu wameongoza usomaji wa Qur’ani kwenye hafla hiyo, wahudhuriaji wamesikiliza Qur’ani kutoka kwa msomaji wa Ataba mbili takatifu bwana Osama Karbalai, na msomaji wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhammad Ridhwa Zubaidi, na bwana Siraji Muniri.

Hafla imehudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru na wapenzi wa kitabu cha Mwenyezi Mungu katika mazingira yaliyojaa utajo wa Mwenyezi Mungu na Ahlulbait (a.s).

Msomaji bwana Siraji Miniri akaimba beti za kumsifu Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Tambua kuwa hafla za Arshu-Tilaawah hufanywa jioni ya kila Ijumaa ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na hurushwa kwenye luninga mubashara kupitia chanel ya Qur’ani tukufu, saa tatu jioni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: