Mwezi kumi na tano Shawwal ni kumbukumbu ya kifo (shahada) ya Hamza bun Abdulmutwalib (a.s) Ammi wa Mtume (s.a.w.w), ambae Mtume alihuzunika sana kwa kifo chake, ulikua mwaka wa tatu hijiriyya.
Alipata shahata (kuuawa) katika vita ya Uhudi iliyo ongozwa na Mtume (s.a.w.w) dhidi ya washirikina wa kikuraishi chini ya uongozi wa Abu Sufiyani.
Riwaya zinaonyesha kuwa Hindu bint Utba -mke wa Abu Sufiyani- alimuambia (Wahshi), ukiweza kumuua Muhammad au Ali au Hamza bun Abdulmutwalib, nitakupa zawadi, akamuahidi kuwa atamuua Hamza.
Wahshi anasema: Wallahi nilikua namuangalia hamza anavyo pangua watu kwa panga lake, hakuna yeyote anayekatisha mbele yake ispokua alimuua, nikashika vizuri mkuki wangu na kumtupia, nikamchoma kiunoni kwake na ukatokeza katikati ya miguu yake, akaanguma, nikamuacha kidogo hadi akafa, na jeshi lake likaishiwa nguvu.
Imepokewa kuwa Hindi aliifuata maiti ya Hamza, akaamuru apasuliwe tumbo lake na akakata ini na kuliweka mdomoni mwake, hakuweza kutafuna akalitema, kisha akakata pua na masikio yake akatemgeneza bangili ya kuvaa mkononi kwake na mkufu wa kuvaa shingoni kwake.
Baada ya kuondoka jeshi la washirikina Mtume (s.a.w.w) alimuagiza Imamu Ali (a.s) akamuambia, nenda kawaangalie kama wamepanda ngamia watakua wanaenda Makka na kama wamepanda farasi wanaenda Madina, naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kama wakienda Madina nitawateka.
Imamu Ali (a.s) anasema: Nikawafuata na kukuta wamepanda ngamia na sio farasi.
Baada ya vita kuisha, Mtume (s.a.w.w) alimchukua Ammi yake Hamza bun Abdulmutwalib na akamzika, kisha akasimama mbele ya kaburi lake huku akiwa analia hadi akazimia.
Mtume (s.a.w.w) alikua anasema: Ewe Ammi wa Mtume wa Mwenyezi Mungu,