Kuhitimisha semina ya Qur’ani inayohusu kanuni za tajwidi katika mkoa wa Najafu

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imehitimisha semina ya Qur’ani katika fani ya tajwidi, iliyofanywa kwenye jengo la Rahmaan katika wilaya ya Mashkhabu, kwa ushiriki wa kundi kubwa la wapenzi wa Qur’ani wanaotaka kukuza uwezo wao, mhadhiri wa hafla ya kufunga semina alikua ni Ustadh Abduridhwa Al-Abuudi.

Kiongozi wa idara ya usomaji katika Maahadi Sayyid Ahmadi Zaamili ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maahadi imezowea kufanya semina za Qur’ani katika mada tofauti wakati wote katika mwaka, hii ni moja ya semina nyingi zinazo fanywa na Maahadi kwa lengo la kukuza uwezo wa usomaji wa Qur’ani, ambapo wamefundishwa usomaji sahihi wa kuzingatia hukumu za tajwidi”.

Akaongeza kuwa: “Semina imedumu kwa zaidi ya miezi miwili, wanafunzi wamefundishwa kwa njia ya (nadhariyya na vitendo), pamoja na kupewa mtihani mwishoni mwa semina kwa lengo la kupima walichovuna kwenye semina hiyo, aidha tumetoa vyeti kwa wote walioshiriki kwenye semina”.

Akamaliza kwa kusema: “Semina zinazofanywa na Maahadi ni sehemu ya harakati zake muhimu, idara ya Maahadi huzipa kipaombele maalum kutokana na faida kubwa inayopatikana kwenye semina hizo, kwani zinasaidia upatikanaji wa wasomi mahiri wenye kufuata hukumu za tajwidi”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Najafu imekua ikifanya semina nyingi za aina tofauti, mamia ya watu wamenufaika katika semina hizo, hutumia uwezo wake wote katika kufundisha fani za Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: