Machapisho ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika maonyesho ya vitabu kimataifa jijini Tehran

Maoni katika picha
Machapisho ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu linalo shiriki kwenye maonyesho ya vitabu ya thelathini na tatu.

Muwakilishi wa kitengo hicho Ustadh Alaa Hamdu Matwar amesema: “Kitengo chetu kimeshiriki kikiwa na mamia ya vitabu vinavyo chapishwa na kitengo pamoja na vituo vya turathi vilivyo chini yetu, ambavyo ni kituo cha turathi za Karbala, kituo cha turathi za Hilla na kituo cha turathi za Basra”.

Akaongeza kuwa: “Ushiriki huu ni sehemu ya harakati za kitengo cha maarifa, zinazolenga kuhuisha turathi za kiislamu na turathi za Ahlulbait (a.s)”, akafafanua kuwa “Sambamba na kuangazia turathi zilizopo kwenye miji tofauti ya Iraq ikiwa ni pamoja na utunzi wa wanachuoni wake”.

Tambua kuwa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu hushiriki kwenye maonyesho tofauti ya vitabu kitaifa na kimataifa, vitabu vyake vinakubalika sana kwenye kila maonyesho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: