Ushiriki wa pekee wa machapisho ya kitengo cha Habari na utamaduni katika maonyesho ya vitabu kimataifa jijini Tehran

Maoni katika picha
Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu linalo shiriki kwenye maonyesho ya vitabu kimataifa jijini Tehran awamu ya thelathini na tatu limepambwa na machapisho mbalimbali ya kitengo cha Habari na utamaduni.

Muwakilishi wa kitengo tajwa Ustadh Ali Mahadi amesema: “Kitengo cha Habari na utamaduni kimeshiriki kwenye maonyesho haya kikiwa na mamia ya vitabu, Pamoja na majarida ya kielimu na mausua za historia na Dini bila kusahau vitabu vya Falsafa na Aqida vinavyo chapishwa na vitengo, vituo na idara zilizo chini yake”.

Akafafanua kuwa: “Umuhimu wa kushiriki kwenye maonyesho ya vitabu ya kitaifa na kimataifa ni kuchangia kujenga uwelewa katika jamii ya kiislamu, na kusambaza fikra na utamaduni wa Ahlulbait (a.s)”. akaongeza kuwa: “sambamba na kutambulisha mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye sekta tofauti”.

Tambua kuwa maonyesho ya vitabu kimataifa yanayo fanyika katika jiji la Tehran kwa mara ya thelathini na tatu, yanafanywa kuanzia tarehe (11 – 21 Mei 2022m).

Kumbuka kuwa kushiriki kwenye maonyesho ya vitabu kimataifa ni moja ya jambo muhimu ambalo Atabatu Abbasiyya hutumia kujitangaza katika ulimwengu wa kiislamu, kwa lengo la kutambulisha mafanikio yake kielimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: