Balozi wa Japani nchini Iraq amesema: Miradi ya Atabatu Abbasiyya ni mizuri na inavutia

Maoni katika picha
Balozi wa Japani nchini Iraq Mheshimiwa Sozuki Kotaru na ugeni aliofuatana nao ametembelea Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Jumatano, na kupokewa na katibu mkuu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini na baadhi ya wajumbe wa kamati yake.

Kisha balozi na ujumbe aliofuatana nao wakatembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wakaanzia kwenye dirisha takatifu na wakatembelea maeneo ya ndani ya ukumbi wa haram tukuru na kuangalia mambo mbalimbali ya kiufundi kisha wakaingia kwenye kamumbusho tukufu ya Alkafeel.

Mwasho wa matembezi yao Mheshimiwa balozi akauambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika inanifurahisha sana kutembelea mji wa Karbala, huu ni miongoni mwa miji muhimu kwa waislamu hapa Iraq, ninafuraha kubwa kutembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na kuangalia baadhi ya miradi yake katika sekta ya ulezi, elimu na ujenzi pamoja na turathi na huduma zinazotolewa kwa mazuwaru na jamii kwa ujumla”.

Akasisitiza kuwa: “Nimefurahishwa sana na miradi tuliyoona, na nitafanya ziara nyingine siku zijazo, ninawapongeza watumishi wa Atabatu Abbasiyya kwa kazi nzuri wanayo fanya, na ninawatakia mafanikio mema”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: