Shindano la makala ya kitamaduni kuhusu mazazi ya Imamu Ridhwa (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya Qur’ani katika ofisi ya maelekezo ya kidini tawi la wanawake chini ya ofisi ya Mheshimiwa katibu mkuu inatangaza shindano la kuandika Makala kuhusu mazazi ya Imamu Ridhwa (a.s) kwa masharti yafuatayo:

  • - Makala ieleze moja ya sehemu katika Maisha ya Imamu Ridhwa (a.s).
  • - Iandikwe vizuri na kupangiliwa taarifa zake kwa ustadi.
  • - Isizidi maneno (500) na isiwe na makosa ya kilugha, vyanzo vyake vitoke kwenye vitabu vinavyo kubalika na kuaminika.
  • - Tarehe ya mwisho ya kupokea Makala hizo ni 1/6/2022m.
  • - Makala zitakazo faulu zitawekwa kwenye vyombo vya mawasiliano ya kijamii na kwenye moja ya majarida mawili ya (Swada raudhataini) au (Riyaadhu Zaharaa).
  • - Washindi watatu wa mwanzo watapewa Abaa na zawadi za kutabaruku kutoka kwenye haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
  • - Mshindi wa nne hadi wa kumi watapewa zawadi za kutabaruku.
  • - Makala zitumwe kwa barua pepe kupitia anuani ifuatayo: alwahdaalqurania@gmail.com.

Au ziwasilishwe moja kwa moja kwenye ofisi ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, sehemu wanapoingilia wanawake katika mlango wa Alqami.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: