Waziri wa afya wa Iraq katika ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu amekutana na katibu mkuu wa Ataba

Maoni katika picha
Waziri wa afya wa Iraq Dokta Hani Al-Aqaabi ametembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika safari yake ya Karbala takatifu jana Jumatano akiwa na ujumbe kutoka wizarani.

Baada ya kumaliza kufanya ziara na kusoma dua, amepokewa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini, wamejadili mambo yanayo husu huduma zinazo tolewa kwa mazuwaru ikiwa ni pamoja na matibabu, hususan katika ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, sambamba na ushirikiano kati yake na idara ya afya ya mkoa wa Karbala.

Kikao hicho kimehudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu Ustadh Jawadu Hassanawi na kiongozi wa ofisi ya kiongozi mkuu wa kisheria Dokta Afdhalu Shami, pamoja na rais wa kitengo cha mahusiano Ustadh Huquqi Muhammad Ali Azharu na mkuu wa hospitali ya Alkafeel Dokta Jaasim Ibrahimi.

Mwisho wa ziara, Waziri akaagwa kwa furaha kama alivyo pokewa, akashukuru sana mapokezi mazuri aliyopewa, akawatakia mafanikio mema viongozi wote na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: