Watumishi wa kitengo cha Imamu Mahadi (a.f) katika mkoa wa Karbala chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wanafanya kazi kubwa ya kutunza jengo la Maqaam takatifu na kulifanya kuwa katika muonekano bora zaidi.
Kiongozi wa kitengo bwana Adnani Dhaifu ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wetu wanafanya kazi kubwa ya kuhudumia mazuwaru wanaokuja kutembelea Maqaam tukufu, na kuhakikisha wanafanya ziara kwa amani na utulivu, sambamba na kutunza jengo tukufu kwa kulifanyia usafi wa mara kwa mara na kuhakikisha linakua katika muonekano mzuri”.
Akaongeza kuwa: “Kutokana na kuongezeka kwa vimbunga vya vyumbi katika mji wa Karbala imetulazimu kuongeza usafi sehemu zote za Maqaam tukufu chini ya utaratibu maalum”.
Akabainishwa kuwa: “Kazi inaendelea vizuri, mabadiliko ya hali ya hewa yamepelekea kuwa na kazi za ziada, ambazo zimeongezwa kwa watumishi wa Maqaam tukufu, kazi zimeongezeka ndani na nje ya Maqaam, kuanzia kwenye kubba takatifu hadi kwenye barabara na maeneo ya karibu yake bila kusahau kumbi zake na kuta za ndani na nje”.
Kumbuka kuwa Maqaam iko upande wa kushoto wa mto Husseiniyya wa sasa katika lango la Karbala la kaskazini, kwenye eneo la mlango wa Salama, kaskazini ya malalo ya Imamu Hussein (a.s) umbali wa (mt 650) takriban, ni mazaru mashuhuri yenye kubba refu, imeitwa kwa jina la Imamu Mahadi msubiriwa (a.f), inasemekana kuwa Imamu Hujjah Mahadi (a.f) aliswali sehemu hiyo katika moja ya ziara zake alizokuja kumtembelea babu yake Imamu Hussein (a.s).