Makamo Rais wa Iran amepongeza tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye maonyesho ya vitabu kimataifa yanayo endelea jijini Tehran

Maoni katika picha
Makamo Rais wa Iran Sayyid Sulat Murtadhwa, ametembelea tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu linalo shiriki kwenye maonyesho ya vitabu kimataifa katika jiji la Tehran kwa mara ya thelathini na tatu.

Sayyid Murtadha ameangalia vitabu vilivyopo katika tawi hilo, akasifu na kupongeza ubora wa elimu iliyopo kwenye vitabu hivyo, jambo ambalo linaonyesha ukubwa wa elimu inayotolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta ya usambazaji wa vitabu.

Tambua kuwa tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu limeshiriki kwenye maonyesho ya vitabu kimataifa katika jiji la Tehran awamu ya thelathini na tatu, likiwa na mamia ya vitambu tofauti sambamba na kufanya shindano la kielimu pamoja na kufungua mlango wa kupokea barua, uliopewa jina la (barua kwa kaburi).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: