Maahadi ya Qur’ani tukuku katika mji wa Najafu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imehitimisha awamu ya pili ya mashindano ya Qur’ani tukufu ambayo wameshiriki wanavyuo (65) wa kiume na wakike.
Mkuu wa Maahadi Ustadh Muhandi Almayali ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mashindano yamefanywa kwa muda wa siku mbili ndani ya kumbi za chuo kikuu cha Kufa, nayo ni sehemu ya mradi wa Maahadi ya Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi, yalikua na sehemu mbili, kila sehemu ilikua na vigezo vyake, sehemu ya kwanza ilikua kwa ajili ya wanafunzi wa kiume na ilikua na washiriki (45) na sehemu ya pili kwa ajili ya wanafunzi wa kike chini ya usimamizi wa Maahadi ya Qur’ani tawi la wanawake katika mkoa wa Najafu”.
Akaongeza kuwa: “Mashindano yalijikida katika mambo mawili, kuhifadhi na maana, kamati ya majaji imetumia njia ya mtandao katika kutoa alama za washiriki, hali kadhalika kiliongezwa kipengele cha kubainisha maneno ya Qur’ani na usomaji wa tenzi kwenye hatua za mwisho za mashindano”.
Akaendelea kusema: “Washindani walikua na kiwango cha juu cha uwelewa wa kufuata maelekezo ya shindano, jumla wa wanafunzi sita wameshinda na kupewa zawadi kwenye hafla ya ufungaji wa mashindano”.
Kumbuka kuwa mradi wa Qur’ani kwa wanafunzi wa vyuo vikuu na Maahadi unahusisha harakati mbalimbali, miongoni mwa harakati hizo ni: Kufanya nadwa za Qur’ani tukufu ndani ya vyuo vikuu, kufanya nadwa kwa wanafunzi wa bweni, kufanya mashindano ya Qur’ani ya kuhifadhi na usomaji, kufanya maonyesho ya Qur’ani na picha, kufanya mashindano ya kuandika Qur’ani, semina za usomaji sahihi wa Qur’ani na kanuni za Tajwidi, ratiba ya kuendeleza walinu wa vyuo vikuu.