Kupiga kura maalum kwa washiriki wa shindano la kitamaduni katika maonyesho ya vitabu kimataifa jijini Tehran

Maoni katika picha
Matawi ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya yanayo shiriki kwenye maonyesho ya jitabu kimataifa katika jiji la Tehran, yamepiga kura maalum kwa washiriki wa shindano la kitamaduni lililoratibiwa na matawi hayo kwenye maonyesho ya vitabu.

Imepigwa kura katika uwanja wa maonyesho na kuhudhuriwa na kundi kubwa la wapenzi wa Ahlilbait (a.s) waliokua wamejaa bashasha.

Kupitia kura hiyo tumepata washindi sita watakaopewa zawadi ya kwenda kufanya ziara katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mji wa Karbala, Ataba mbili tukufu zitasimamia safari yao.

Washindi wamepewa pia zawadi za kutabaruku kutoka kwa bwana wa mashahidi na ndugu yake mnyweshaji wenye kiu Karbala (a.s).

Shindano lilikua na maswali mengi ya kihistoria yaliyoandikwa kwenye karatasi na kuwekwa kwenye masanduku baada ya washiriki kuandika majibu.

Shindano hili ni moja ya harakati muhimu za Ataba mbili tukufu kwenye maonyesho haya, limepata muitikio mkubwa kutoka kwa wadau wa maonyesho.

Mashindano haya ni sehemu ya malengo ya Ataba mbili tukufu ya kutangaza fikra za Ahlulbait (a.s) na kujenga utamaduni wa kujua Dini, Historia na mambo ya kijamii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: