Hivi karibuni kituo cha turathi za Basra chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetoa (kitabu kinachoeleza matukio ya kuuawa kwa Maimamu wa Ahlulbait a.s) kilicho andikwa na Dokta Rahim Halo Muhammad.
Kitabu hicho ni moja ya machapisho ya kituo, kimeandika mambo mengi kutoka sehemu tofauti kwenye vitabu vya historia na sira vinavyo kubalika, kimeandika uonevu mkubwa walio fanya watawala wa umma huu kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) kuanzia kwa kiongozi wa waumini Ali (a.s).
Muandishi wa kitabu amekiweka kwa milango, kila mlango unaeleza tukio la kuuawa mmoja wa Maimamu watakatifu, sambamba na kuandika kwa ufupi utambulisho wa kila Imamu, kuanzia jina, nasaba, tarehe ya kuzaliwa na sehemu aliyo zaliwa, utambulisho wa mama, nasaba yake, jina la kuniya, idadi ya Watoto, wake, hadi kufikia tukio la kifo chake, kwa njia ya kielimu yenye misingi ya matokeo.
Kumbuka kuwa kituo tajwa kinaorodha kubwa ya vitabu tofauti, na vingine vipo katika hatua ya uchapishwaji vitatoka hivi karibuni, bila shaka vitakua na mchango mkubwa katika maktaba za kiislamu.