Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya, imeanza kusajili washiriki wa semina za majira ya joto kwa vijana wenye umri wa miaka (7 hadi 15).
Huduma zote zinatolewa bure kwenye semina, watafundishwa (usomaji wa Qur’ani, kuhifadhi, Aqida, Fiqhi, Akhlaq na Sira), Pamoja na ratiba za kitamaduni na kiburudani, ratiba zote zitasimamiwa na wataalamu wenye weledi mkubwa.
Usajili unafanywa kwa kwenda moja kwa moja kwenye kamati ya usajili iliyopo katika shule ya Al-Ameed, kuanzia saa mbili asubuhi hadi hadi saa kumi na mbili jioni, njoo na picha ya mwanafunzi, usajili umeanza tarehe 21 Mei 2022m, hadi tarehe ishirini na saba mwezi huo.
Kumbuka kuwa mradi huu ni sehemu ya kuchangia kueneza kwa utamaduni wa kusoma Qur’ani kwa vijana wanaochibukia, aidha ni sehemu ya kufanyia kazi kauli ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) isemayo: (Wafundisheni Watoto wenu mambo matatu: Kumpenda Mtume wenu na kuwapenda watu wa nyumbani kwake na Qur’ani tukufu), semina hii hufanywa kila mwaka baada ya kukamilika msimu wa masomo, wamehitimu semina hizi maelfu ya wanafunzi.