Atabatu Abbasiyya tukufu imejenga kituo cha kusafisha maji kwa ajili ya wakazi na mazuwaru

Maoni katika picha
Idara ya maji chini ya kitengo cha miradi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imemaliza ujenzi wa kituo cha kusafisha maji (R.O station) katika moja ya sehemu za utoaji wa huduma katika barabara ya (Baabil – Karbala), kwa lengo la kuhakikisha maji safi na salama ya kunywa yanapatikana kwa wakazi wa eneo hilo na mazuwaru wanaotumia barabara hiyo.

Kiongozi wa idara ya maji Mhandisi Basaam Hashimiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kituo hicho kinauwezo wa kuzalisha lita 2000 kwa saa, kinamitambo ya kisasa, sambamba na mahodhi makubwa ya kutunzia maji kulingana na mahitaji”

Akaongeza kuwa: “Kituo hiki kitasaidia wakazi wa maeneo haya, ukizingatia kuwa maeneo haya yanauhaba mkubwa wa maji safi ya kunywa, kituo kipo kwenye barabara inayotumiwa na mazuwaru wengi, na huwa kuna mawakibu nyingi za kutoa huduma, hivyo kituo kitasambaza maji kwa maukibu hizo, hususan wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu, ambapo huwa kuna matumizi makubwa ya maji”.

Kumbuka kuwa hiki ni moja ya vituo vingi vilivyo jengwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ndani na nje ya mkoa wa Karbala, miji Minji yenye shida ya maji imenufaika kupitia vituo hivyo, tumeshajenga zaidi ya vituo (25) vyenye uwezo tofauti kulingana na mahitaji ya kila sehemu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: