Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu limekamilisha ushiriki wake kwenye maonyesho ya vitabu kimataifa jijini Tehran

Maoni katika picha
Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu limekamilisha ushiriki wake kwenye maonyesho ya vitabu kimataifa jijini Tehran awamu ya thelathini na tatu.

Tawi limepata muitikio mkubwa kutoka kwa wadau wa maonyesho, wamefika kwenye tawi hilo kuangalia vitabu vinavyo chapishwa na Ataba tukufu, kupitia kitengo cha elimu na kitengo cha maarifa ya kiislamu.

Aidha tawi hilo limeendesha shindano la kitamaduni kwa kushirikiana na tawi la Atabatu Husseiniyya, ambapo jumla ya washiriki sita wamefaulu na kuzawadiwa kwenda kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Tawi lilikua na proram nyingine iliyopewa jina la (barua kwa kaburi), watu waliotembelea tawi hilo wameandika barua za kupeleka kwa bwana wa mashahidi na mbeba bendera wake (a.s).

Mafanikio ya program hii ni muendelezo wa mafanikio yaliyopatikana kwenye program zilizo tangulia.

Kumbuka kuwa kushiriki kwenye maonyesho ya vitabu ya kimataifa ni moja ya sehemu ya kuitambulisha Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye ulimwengu wa kiislamu, na kutambulisha mafanikio yake kielimu na machapisho yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: