Kitengo cha mahusiano kimeanzisha program ya (tambua zaidi) kwa watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha mahusiano katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanzisha program ya (tambua zaidi) kwa watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa lengo la kuangalia huduma zinazo tolewa na miradi ya Ataba tukufu kwa mazuwaru na wananchi.

Msimamizi wa program hiyo Ustadh Rasuul Twaaiy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa “Hii ni moja ya program zinazo endeshwa na kituo, katika mambo yanayo husu wageni wa Atabatu Abbasiyya tukufu au watumishi wake, hii ni program ya kutembelea miradi ya Atabatu Abbasiyya na huduma zinazo tolewa na Ataba”.

Akaongeza kuwa: “Utembeleaji wa miradi ya Ataba ni sehemu ya kuwajulisha watumishi miradi hiyo, na manufaa yayopatikana sambamba na kujenga uhusiano baina ya watumishi wa vitengo tofauti”.

Akamaliza kwa kusema: “Matembezi (jaula) yamehusisha maeneo tofauti, wamesikiliza maelezo ya hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi na malengo ya miradi hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: