Maukibu ya watu wa Karbala inaelekea kwenye malalo ya Imamu Ridhwa na dada yake Maasuma (a.s)

Maoni katika picha
Maukibu ya watu wa Karbala inaelekea katika malalo ya Imamu Ridhwa na dada yake Maasuma (a.s), kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha Imamu Swadiq (a.s), aliyekufa mwezi ishirini na tano Shawwal.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Sayyid Aqiil Abdulhussein Alyasiriy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika Maukibu ya watu wa Karbala imezowea kuadhimisha matukio ya kidini ndani na nje ya mkoa wa Karbala, ikiwa ni pamoja na kuhuisha tukio hili la kifo cha Imamu Swadiq (a.s) ndani ya malalo takatifu ya Imamu Ridhwa na dada yake Sayyidah Maasuma (a.s), maandalizi ya kufanya ibada ya uombolezaji na utoaji wa huduma yamekamilika”.

Akaongeza kuwa “Kituo cha kwanza cha maukibu kitakua kwenye malalo ya bibi Maasuma bint wa Imamu Alkadhim (a.s) katika mji mtukufu wa Qum, Kisha maukibu itaelekea katika mji wa Mash-had kwenye malalo ya Imamu Ridhwa (a.s).

Akabainisha kuwa: “Kuna ratiba ya uombolezaji iliyo andaliwa kwa ajili ya msiba huu, inavipengele vingi, miongoni mwa vipengele vyake ni: kuwasili wa maukibu za kuomboleza katika malalo mbili takatifu, sambamba na kutoa huduma ya chakula kwa waombolezaji na kufanya majlisi za kuomboleza katika husseiniyya tofauti ndani ya mji mtukufu wa Qum na Mash-had”.

Kumbuka kuwa watu wa Karbala wamezowea kufanya majlisi kama hii kila mwaka, chini ya usimamizi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, sambamba na kufanya kila wawezalo katika kurahisisha utekelezaji wa ratiba ya kuomboleza kwenye matukio tofauti ya uombolezaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: