Wataalam wa uokozi na mafunzo wa kitabibu chini ya kitengo cha uboreshaji na maendeleo endelevu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wameanza kutoa semina za program ya (katika kila nyumba muokozi) baada ya kusimama kwa mwezi mzima wa Ramadhani.
Mmoja wa wakufunzi wa semina hiyo bwana Kabtan Sefu Abbasi, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa “Semina hii ni maalum kwa watumishi wa Atabatu Abbasiyya wanaotoa huduma moja kwa moja kwa mazuwaru, ni miongoni mwa semina muhimu”.
Akaongeza kuwa: “Semina inalenga kuandaa nguvu kazi ya kutosha katika uokozi na utoaji wa huduma ya kwanza, wenye uwezo ya kupambana na majanga, wanafundishwa namna ya kuokoa Maisha ya mtu wakati wa majanga sawa awe zaairu au raia wa kawaida”.
Akafafanua kuwa: “Semina hizi wanafundishwa kwa (nadhariyya na vitendo), kunamada tofauti zinazofundishwa, kama vile: matatizo ya moyo, kwa watu wazima na watoto na zinginezo”.
Akasisitiza kuwa: “Ni muhimu sana mbinu za uokozi zijulikane vizuri na kila mtu, ni muhimu kujua mbinu za uokozi kwa ujumla kwa ajili ya kutoa huduma hiyo kwa watumisha au mazuwaru”.
Tambua kuwa wataalam wa uokozi na mafunzo ya kitabibu, huendesha semina mbalimbali za aina hii katika kipindi chote cha mwaka, wamesha hitimu makumi ya watumishi na wako tayali lutoa huduma katika jamii.