Mkuu wa mkoa wa Karbala na Najafu katika ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Jana siku ya Jumatano baada ya Adhuhuri mkuu wa mkoa wa Karbala mhandisi Jasim Khatwabi akiwa na mkuu wa mkoa wa Najafu Dokta Majidi Alwaaili wametembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Baada ya kufanya ibada ya ziara na kusoma dua wamekutana na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Mustwafa Murtadhwa Dhiyaau-Dini, amewakaribisha wageni na kubadilishana nao mawazo, wameongea kuhusu namna ya kutoa huduma bora kwa mazuwaru wanaokuja kumtembelea Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na namna ya kushirikiana kwa ajili ya kufanikisha swala hilo, hali kadhalika wakajadili baadhi ya miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu inayosaidia kuhudumia mazuwaru.

Kikao hicho kilihudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Ustadh Jawadi Hasanawi na rais wa kitengo cha mahusiano Ustadh Muhammad Ali Azharu, pamoja na bwana Fadhil Auzi kutoka Atabatu Husseiniyya.

Mwisho wa kikao hicho, ugeni umetoa shukrani za dhati kwa mapokezi mazuri waliyopewa, na kuwatakia mafanikio mema wahudumu wote wa malalo hii takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: